Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.

00:00
00:00

Resumen del episodio

Madai ya mengine kuitaka serikali kusitisha mipango yoyote ya kutenga maeneo ya misitu kwa ajili ya matumizi mengine, kama vile ujenzi wa Barabara, kudumisha marufuku ya ukataji miti ili kulinda misitu iliosalia nchini Kenya, Chukua hatua za haraka na thabiti dhidi ya shughuli za ukataji miti kinyume cha sheria na uporaji wa ardhi ndani ya maeneo ya misitu

Episodios

263-

Kenya: Sahihi elfu sitini za kuitaka serikali kusitisha ukataji wa miti kwenye misituya umma

Madai ya mengine kuitaka serikali kusitisha mipango yoyote ya kutenga maeneo ya misitu kwa ajili ya matumizi mengine, kama vile ujenzi wa Barabara, kudumisha marufuku ya ukataji miti ili kulinda misitu iliosalia nchini Kenya, Chukua hatua za haraka na thabiti dhidi ya shughuli za ukataji miti kinyume cha sheria na uporaji wa ardhi ndani ya maeneo ya misitu

12 oct. 2026
262-

Wanaharakati wa mazingira walalamikia athari za kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote Lamu

Licha ya faida za kiuchumi, mashirika ya mazingira na wanaharakati wa mazingira wanasema kiwanda hicho ni tishio kwa mifumo ikolojia ya eneo la Pwani pamoja na riziki ya jamii katika eneo hilo. Pamoja na Omar Elmawi, wakili wa mazingira na nishati kutoka Mombasa, tunajadili mradi huu wa Dangote ambao ujenzi wake unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 40 ijayo.

05 oct. 2026
261-

Je unafahamu umuhimu wa kuzuia upotevu na uharibifu wa chakula?

Mwaka huu ni maadhimisho ya saba ya siku ya kimataifa ya kutoa hamasisho kuhusu utupaji na upotevu wa chakula, ambao unachangia kati ya asilimia 8–10 ya utoaji wa gesi joto Lengo la maendeleo endelevu nambari 12.3 linalenga kuona dunia ikipunguza upot’evu na uharibufuwa chakula kwa nusu ifikapo mwaka 2030.

28 sep. 2026
260-

Septemba 22, siku ya kimataifa ya kutotumia magari mijini

Wananchi katika miji mbalimbali ya dunia wanahimizwa kuacha magari yao binafsi nyumbani na kukumbatia mbinu zingine za usafiri zilizo endelevu kama kutumia baiskeli au kutembea kwa miguu. Makala haya yanaangazia namna baiskeli za umeme zinaweza kuwa moja ya suluhu ya uchafuzi wa hewa kwenye miji unaotokana na sekta ya usafiri.

23 sep. 2026
259-

Kenya: Wanaharakati watoa mapendekezo mapya dhidi ya plastiki zinazochafua mazingira

Kenya inakabiliwa na changamoto ya plastiki zinazotumiwa mara moja tu kama vile mifuko inayotumiwa sokoni kupakia mboga ambazo huchangia katika uchafuzi wa mazingira licha ya kupigwa marufuku. Ni Kutokana na hili ambapo wanaharakati wa mazingira wamekuja na mapendekezo mapya ya kukabiliana na tatizo hili, mbali na suluhu la uchakataji. Moja ya matokeo ya mapendekezo haya ni kuiweka Kenya katika nafasi ya uongozi wa kikanda katika uvumbuzi wa mifumo ya kutumia tena bidhaa. Hellen Kahaso Dena kutoka shirika la Greenpeace Africa amechambua swala hilo. Sikiliza zaidi kwa kubofya.

14 sep. 2026